JESHI LA POLIS MKOANI TANGA,LITAKIWA KUONGEZA BIDII KATIKA MAJUKUMU YAKE

Jeshi la polis mkoani tanga,limetakiwa kuongeza bidii katika majukumu yake ili waweze kutokomeza kabisa wimbi la biashara ya wahamiaji harama sanjari na uingizwaji na matumizi ya madawa ya kulevya mkoani hapa.


Mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa tanga,ambae ni mkuu wa wilaya ya muheza,mhandisi mwanaasha rajabu tumbo ametoa kauli hiyo katika maadhimisho ya siku ya usalama barabarani iliyoadhimishwa kimkoa katika viwanja vya tangamano jijini hapa. 

Mwanaasha tumbo amesema bado maeneo mbalimbali ya mkoa wa tanga yanatawaliwa na vitendo hivyo ambavyo ni hatari katika jamii ambapo amewaagiza askari wa jeshi la polis ama kamati ya ulinzi na usalama kwa ujumla kuona namna gani kushikamana kupiga vita vitendo hivyo.

Aidha,tumbo amewataka wananchi kuwafichua wote wanaojiusisha na vitendo hivyo katika kaya zao huku akitoa wito kwa wazazi na walezi kuwafunda watoto wao ili wajiepushe kushiri kwenye masuala hayo. 

Kwa upande wake kamanda wa jeshi la polis mkoa wa tanga,kamishina msaidizi mwandamizi wa jeshi la polis,sacp eduard bukombe amemuhakikishi kiongozi huyo kuwa wamejipanga kikamilifu kukabiliana na vitendo vyote visivyokubalika kisheria na kutoa ovyo kwa wote wanaojiusisha na vitendo hivyo kuacha mara moja kwani mkono wa sheria unawajia.

No comments