ACT - Wazalendo watangaza mikakati ya mwaka 2018


Chama cha ACT Wazalendo kupitia Katibu wake wa Itikadi, Ado Shaibu kimetangaza mikakati yake mipya ya mwaka 2018 ikiwemo kuimarisha ushirikiano na vyama vingine vya upinzani hususan katika mapambano dhidi ya Demokrasia na kudai Katiba Mpya.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Jumapili jijini Dar es Salaam, ambapo amesema mbali na mkakati wa ushirikiano na vyama hivyo vya siasa, wamejipanga pia kujenga uhusiano mzuri na vyama vya wafanyakazi wa taasisi mbalimbali nchini lengo likiwa ni kukabiliana na changamoto zinazowakabili.


“Tumeshakwisha viandikia barua vyama vya wafanyakazi na tumepanga kufanya ziara katika ofisi za vyama hivyo.” Alisema Shaibu.


Chama hicho pia kimetangaza kuanza mchakato wa uchaguzi wake wa ndani ya chama kuanzia ngazi ya matawi na kilele cha uchaguzi huo kitakuwa ni mwezi Agosti mwaka huu.
Katika kusisitiza hilo, Katibu mwenezi huyo amesema, tayari wameshawaalika wanachama wake kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali zilizopo ndani ya chama hicho.

No comments