MJUE KOCHA AJAYE WA SIMBA SC- HUBERT VELUD
Huyu ndio kocha mpya
aliyeletwa nchini na Boss wa wekundu wa Msimbazi bilionea Mohamedi Dewji
akitokea nchini Ufaransa.
Hubert Velud alizaliwa
tarehe 8 Juni, 1959 katika mji wa Villefranche-sur-Saône mashariki mwa nchi ya
Ufaransa.
Historia yake kisoka
kocha huyu mwenye uzoefu mkubwa na soka la Afrika, alianza kucheza soka kama
mlinzi wa kati katikati ya miaka ya 70 kabla yakuamua kuwa golikipa akiwa na
klabu ya Stade Reims ambayo alidumu nayo mpaka mwaka 1989.
Mwaka 1989 aliingia
mkataba na klabu ya Charlons sur Marne ambayo alidumu nayo kwa miezi 11 tu
kabla yakuamua kustaafu soka na kujikita katika masuala ya ukocha.
Ana leseni daraja A ya
ukocha inayotambuliwa na Shirikisho la soka barani Ulaya ( UEFA ) .
UZOEFU AFRIKA
Hubert Velud ni mzoefu
na soka la Afrika akikumbukwa jinsi alivyoweza kukiweka sawa kikosi cha timu ya
taifa ya Togo mwaka 2009-10 alipokuwa akikinoa.
2011 Velud aliingia
mkataba na klabu ya ligi kuu nchini Morocco klabu ya Hassania Agadir ambayo
aliiwezesha kuwa ndani ya nne bora ya msimamo wa ligi. Mwaka 2012 mwanzoni
matajiri wa ES Setiif toka nchini Algeria walimnyakua kocha huyu kuja kuinoa
klabu hiyo. Akitumia mfumo wake maarufu wa 4-3-3 aliweza kuwapa ubingwa wa ligi
kuu ( League one ) msimu wa 2012-13.
Akiwa amewakatia
tiketi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa Afrika wapinzani wao USM Alger
walimnyakua mfaransa huyu ili kuimarisha ushindani kitu ambacho kiliwaudhi
Setiif na waliyumba kiufundi. Velud aliweza kuwapa kombe la Algerian Super Cup
katika kipindi kifupi tu hali iliyozidisha ubora wa soka lake Afrika.
2015 aliachana na USM
Alger baada ya kupata ofa nono ya wakali wengine wa ligi ya Algeria CS
Constantine moja ya timu kongwe sana nchini humo ikiundwa mwishoni mwa karne ya
19. Hawa alikaa nao kwa miezi 8 akianza kukisuka upya kikosi hicho ambacho
msimu wa 2014-15 kiliondokewa na nyota wake wengi. Akiwa katikati ya msimu
bilionea Moise Tchitumbi wa TP Mazembe alimwekea ofa kubwa mezani ili akiongoze
kikosi chake katika michuano ya klabu bingwa Afrika na ligi za ndani baada ya
kusikia ubora wake .
Alijiunga na TP
Mazembe mwaka 2016 na kuwapa ubingwa wa Linafoot na Super Coupe du Congo.
Yalikuwa mafanikio ya haraka na wakali hao wa Lubumbashi lakini hakuweza kudumu
nao baada ya timu za Afrika kaskazini kutupa tena ndoano yao kumnasa kocha huyo
aghali!.
Etoille du Sahel
wanaoshiriki ligi kuu nchini Tunisia walimnasa kocha huyu kwa msimu wa 2016-17
ingawa hakuwa na mafanikio makubwa sana na klabu hiyo hali iliyomfanya mwishoni
mwa msimu kutimkia kwao nchini Ufaransa.
Huyu ndio Hubert Velud
ambaye Simba wamemleta nchini kukinoa kikosi chao katika harakati za kuusaka
ubingwa wa ligi Tanzania na ushiriki wao katika michuano ya kombe la Shirikisho
barani Afrika.
Ni kocha ambaye
anahusudu soka la vijana, kasi , nguvu , pasi fupi fupi zenye kasi katika kushambulia
akiwa muumini mkubwa Total football. Mkali sana katika masuala ya nidhamu na
yupo radhi kuvunja mkataba wake pale anapoingiliwa majukumu yake akihofia
kuharibiwa CV yake.
Moja ya tukio la
kusikitisha kwa kocha huyu ni mwaka 2010 akiwa na timu ya taifa ya Togo katika
michuano ya AFCON nchini Angola pale timu ya taifa ya nchi hiyo iliposhambuliwa
na waasi alipigwa risasi mkononi
Post a Comment