Mvua zakwamisha mradi wa maji wilayani MUHEZA.


Mvua zilizonyesha mwezi mei mwaka jana wilayani Muheza zimepelekea changamoto katika kufanikisha utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa maji kutoka mto zigi hadi kijiji cha Mlingano.

Mkurugenzi mtendaji wa halmshauri ya wilaya ya Muheza mkoani TANGA,Bi.LUIZA MLELWA ameyasema hayo ofisini kwake wakati alipokua akizungumza na MAJLIS MEDIA kuhusu utekelezaji wa mradi huo.

Akizungumzia mradi huo BI.LUIZA amesema kwamba ujenzi wa mradi huo umeanza kutekelezwa mwezi july,2015 na ulitakiwa kukamilika mnamo tarehe 30 marchi,2017,ambapo mradi huo unatekelezwa na mkandarasi White City International kwa kushirikiana na kampuni ya Yumde Construction zote za jijini Dar es salaam na kusema kuwa unatarajia kutumia gharama za Tsh.Bilioni 1, 594, 235,046.

Amesema miongoni mwa kazi walizofanikiwa kuzifanya katika mradi huo kwa mwaka jana ni uchimbaji wa mtaro kutoka mto ziggi hadi kwenye tank la kizoto pamoja na mitaro ya usambazaji maji na kulazia bomba katika njia kuu na ulazaji wa bomba katika vijiji vinne kibaoni,mlingano,muungano pamoja na upare.

Pia ni pamoja na kufanikiwa ujenzi wa sump tank,ujenzi wa chanzo cha maji (Intake),kuvuta umeme wa njia tatu hadi katika nyumba ya mitambo,ujenzi wa nyumba ya mtambo,ujenzi wa vituo 30 vya kuchota maji,ujenzi wa tank la lita 45,000 katika kitongoji cha kizota kijiji cha mlingano sanjari na ujenzi wa tank lita 90,000 katika kitongoji cha upare.

Aidha,amesema walishidwa kufikia lengo la kukamilisha mradi huo mwaka jana kutokana na uwepo wa changamoto ya uharibu mkubwa uliojitokeza kwenye kingo za chanzo cha maji cha mto ziggi zilizosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha wilayani humo ambapo zilisababisha miti mikubwa kuanguka na kuziba kitorosha maji na kupelekea maji kutafuta njia mbadala ya kusafiri pembezoni mwa mto huo.

Amesema hadi kufikia tarehe 30.06.2017 mwaka jana jumla ya fedha kiasi cha Tsh.Bilioni 1,423,565,115 kimetumika kumlipa mkandarasi M/s White City International Contractor & Yumde Construction Company Ltd (JV).na chanzo cha pesa ni hizo kimetoka kwa wahisani wa Water Sector Development Program (WSDP).

Awali amesema kuwa halmashauri yake imekwishaanza marekebisho katika sehemu ya chanzo iliyoharibiwa tangu mwezi December mwaka jana.

Mapema mkurugenzi huyo wa halmashauri ya wilaya ya muheza mkoani TANGA,BI.LUIZA MLELWA ameema kwamba mradi huyo unatarajiwa kufaidisha maeneo ya kata ya Mlingano na kata ya Pande Darajani ambayo ni kibaoni,kizota,kwebago,vanga,mission,machemba,kilapula,mkulumuzi,Azimio1 na Azimio11,Mzambarauni,Mji mwema sanjari na Dilima na pia amesema mradi huo una mtambo wa bomba wenye urefu wa mita 47,000 na kuongeza kwamba kukamilika kwa mradi huo unatarajiwa kuhudumia watu wapatao 7,165 kutoka katika maeneo tajwa hapo awali.


No comments