Askari wawili wafariki Dunia mkoani Mbeya
Gari aina ya Landrover
mali ya Jeshi la Polisi kikosi cha kutuliza ghasia mkoa wa Mbeya yenye no PT.2079
likiendeshwa na askari no. G.3452 PC Adam miaka 30, iliacha njia na kupinduka wakati linawapeleka askari kazini leo Alhamisi january18. 2018 majira ya saa kumi
na dakika 45 jion maeneo ya Iwambi barabara ya Mbeya Tunduma kata ya Iwambi
tarafa ya Iyunga jiji na Mkoa wa Mbeya na kusababisha vifo vya askari wawili
ambao ni
H.1215PC Prosper s/o Jordan Chalamila miaka 29, wa FFU Mbeya na
1.
H.4335 PC Mathew
s/o Jailos Mpogole miaka 26, wa FFU Mbeya
Na Kujeruhi askari wengine
9 ambapo kati yao watatu wamelazwa katika hospitali ya rufaa Mbeya;
1.
G.3452 PC Adam
miaka 30, ambaye ameumia maeneo ya kifua
2.
G.6849 PC Khamis
Ally miaka 32, ambaye ameumia maeneo ya kichwani.
3.
H. 6952 PC Kelvin
s/o Martini miaka 28, ambaye ameumia maeneo ya kichwani/ usoni
Askari wengine 06,
Walitibiwa na kuruhusiwa ambao ni;
1.
H.3929 PC Leonard
Michael miaka 26, Alipata jeraha mkono wa kushoto.
2.
H.469 PC Fredy
Mbande miaka 28, alipata jeraha mgongoni.
3.
H.948 PC David
Ibrahim miaka 27, alipata maumivu ya mwili.
4.
G.9588 PC Marwa
Itembe miaka 29, Alipata maumivu ya mwili.
5.
H.1325 PC
Christopher Daniel Msangi miaka 26, alipata maumivu ya mbavu.
6.
H.6789 PC Lucas
Andrea Mashala miaka 24, ambaye alipata jeraha kichwani kulia na maumivu ya
mbavu kulia.
Miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya rufaa Mbeya huku Chanzo cha
ajali kikitajwa kuwa ni mwendo kasi
Post a Comment