Licha ya Rais maguful kupiga stop michago mashuleni bado korogwe vijijini wachangishwa kila mzazi 53,600
KOROGWE.
Wananchi wa Tarafa ya
MAGOMA,halmashauri ya KOROGWE vijijini mkoani TANGA,wamepaza sauti zao kwa
kuiomba serekali kuwasaidia kuweza kurudishiwa fedha zao walizochangishwa
kwaajili ya watoto wao waliojiunga na kidato cha kwanza.
Mapema wakizungumza na MAJLIS
MEDIA hii leo kwa hisia kali wananchi
kutoka maeneo ya MAGOMA,MASHEWA na FOLOFOLO,wameanza kwa kutoa shukuran kwa
mheshimiwa Rais magufuli kupiga marufuku michango mashuleni, na kuongeza kwamba
licha ya marufuku hiyo lakini katika tarafa yao wamekwishachangishwa fedha
kwaajili ya utengenezaji wa madawati ambapo wamedai kuwa kwa kila mzazi wa
mtoto wa kidato cha kwanza ametoa shilingi 31,000 na wengine elfu 53,600.
Aidha,wamesema kuwa
kutokana na maisha kuwa magumu kwa upande wao sasa ni wakati wakuweza kurudishiwa
fedha hizo ili waweze kumudu gharama za maisha kwenye kaya zao wanazoishi.
Kwa upande wake Diwani wa
kata ya folo folo ABDALLAH HASSANI MDOE amekiri wananchi wake kuchangishwa
michango hiyo kutokana na changamoto ya upungufu wa madawati katika shule ya
sekondari ndani ya tarafa hiyo.
Awali,MJLIS MEDIA
imelazimika kumtafuta mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Korogwe Vijijini Ndugu.GEORGE
JOHN NYARONGA,ambapo kwa upande wake amesema kwamba ofisi yake haijatoa kibali
chochote cha mzazi kuchangishwa michango mashuleni huku akiahidi kulifuatilia
suala hilo kujua undani wake.
Halikadhalika
Ndugu.GEORGE NYARONGA amewatahadharisha
watumishi wa masula ya elimu katika halmashauri hiyo kufanya kazi kwa uandilifu
kwa kutojiusisha na masuala ya ujanja ujanja sanjari na uongo katika nyazifa zao
hili waweze kujipatia fedha kwa kuwa hil ni kosa kisheria na maadili ya
utumishi bora.
Post a Comment