Mamia ya wananchi Tanga wafurika misikitini
Makundi
kwa makundi ya wananchi wa halmashauri ya jiji la tanga,hii leo wamefurika
katika misikiti mbalimbali iliopo jijini hapa kwaajili ya kuweza kujipatia
huduma ya maji katika misikiti hiyo.
Mwanahabari mwandamizi
wa majlis media ameyabainisha hayo wakati aliopofanya ziara endelevu ya
ufuatiliaji wa hali ya huduma ya maji katika jiji la tanga.
Hayo yamejitokeza kufuatia
jiji la tanga kukumbwa na tatizo la ukosefu wa huduma ya maji safi na salama kutoka
kwa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira tanga uwasa toka mwezi january
kuanza mwaka huu
Miongoni mwa maeneo ya
misikiti iliotembelewa na mwanahabari wa majlis leo na kukuta makundi ya wananchi
wakifuata huduma hiyo ya maji ni msikiti wa Ibadhi bara bara ya 12,mabawa,shamsil
maarif islamiya duga,msikiti wa mchuzi wa nyoka,magomeni na mingineo.
Wakizungumza na
mwanahabari wa majlis media wananchi hao ambapo asilimia kubwa ni wakinamama
wamesema kwamba wanapata adha lukuki katika kaya zao kutokana na ukosefu wa
huduma hiyo muhimu katika maisha ya binadamu.
Aidha,wametaja athari
zilizojitokeza katika kaya zao kutokana na tatizo la ukosefu wa maji kuwa ni
kushindwa kufanya kazi za uchumi kutokana kutumia muda mwingi kutafuta huduma
ya maji,kutumia gharama kubwa kununua maji ya dukani kwaajili ya mahitaji ya
nyumbani,kuumwa homa za matumbo kutokana na kutumia maji ambayo si salama
kutoka visimani.
Awali wananchi hao
wameiomba serekali kupitia wizara ya maji na umwagiliaji kuboresha huduma za
upatikanaji maji kwa kua hivi sasa mamlaka hiyo imezidiwa na wateja wa huduma
hiyo hali inayosababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi.
Post a Comment