Wazazi wilayani Lushoto wawaamuru watoto kujaza majibu ya uongo mtihan darasa la7

Baadhi ya wazazi wilayani LUSHOTO mkoani TANGA,wametajwa kuwa ni chanzo cha kufeli kwa baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba kwa kuwaamuru kujaza majibu ambayo si sahihi katika mitihani ya taifa kwa lengo la kukwepa mahitaji ya shule pindi watoto wao wanapopaswa kujiunga na kidato cha kwanza.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Lushoto KAZIMBAYA MAKWEGA ameyasema hayo hiii leo wakati alipokua akizungumza kwa njia ya simu na mwanahabari wa MAJLIS MEDIA.

KAZIMBAYA amesema kwa kipindi cha mwaka jana hali hiyo ilishamiri katika halmashauri yake jambo ambalo amesema lilishusha kwa kiasi fulani hali ya ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba ambapo ametoa onyo kali kwa wazazi kuacha mara moja mchezo huo.

Aidha,katika hatua nyengine mkurugenzi huyo ameizungumzia hali ya mwitikio wa wazazi kuwapeleka watoto wao kujiunga na darasa la awali ambapo amesema kwa mwaka huu mwitikio ni mkubwa kuliko mwaka jana katika kipindi hiki cha mwezi January.

Mkurugenzi KAZIMBAYA amesema kwa sasa shule nyingi za msingi katika hamashauri yake zina changamoto ya miundombinu ya madarasa hali inayowalazimu baadhi ya wanafunzi kurundikana kwa wingi kwenye madarasani.




No comments