RPC TANGA,Zoezi La Ukaguzi Wa Magari Ni Endelevu
Jeshi la polis mkoani TANGA,limesema zoezi la ukaguzi wa magari
mbalimbali mkoani hapa ni endelevu huku
ikielezwa kwamba lengo kubwa la zoezi hilo ni kuweza kubaini uwepo wa vyombo
vya moto vinavyokiuka sheria na kanuni za usafiri.
Aidha,BUKOMBE amesema kuwa mwishoni mwa mwaka jana (2017) walifanikiwa
kufanya kaguzi za mara kwa mara katika magari mbalimbali na kubaini uwepo wa
tatizo kubwa la matumizi mabaya ya vyombo vya usafiri barabarani sambamba na
uwepo wa magari mabovu ambapo amesema agenda hiyo ni endelevu na hivi sasa
amekwisha liagiza jopo la wakaguzi waliobwebwea kuendelea na zoezi hilo mkoani
hapa.
Katika hatua nyengine kamanda huyo ametoa onyo kwa wamiliki wa
magari,madereva sambamba na wananchi kwa ujumla kufuata sheria za usalama
barabarani na kusema katika uongozi wake hatomfumbia macho mtu yeyote anaekiuka
sheria hizo.
Awali,Kamanda BUKOMBE amezungumzia suala la utendaji kazi wa vituo vya
polis mkoani Tanga ambapo amesema utendaji ni mzuri na kuongeza kuwa mikakati
aliyonayo kwa sasa ni kutengeneza mfumo mzuri kati ya wananchi na jeshi la
polis kwa lengo la kutokomeza kabisa malalamiko yanayotolewa na wananchi dhidi
ya wahudumu wa jeshi hilo katika vituo hivyo.
Pia amesema anatarajia kufanya ziara za mara kwa mara katika vituo vyote
vya polis ili aweze kubaini uwepo wa askari wa jeshi hilo ambao si waadilifu
katika majukumu yao na kutoa rai kwa askari wa jeshi polisi mkoani hapa kufanya
kazi kwa kuzingatia maadili ya utumishi bora wa viongozi wa umma nchini.
Post a Comment