Serikali imeagiza zao la Mbaazi lianze kuliwa katika Magereza na shule
Serikali imeagiza zao la Mbaazi lianze kuliwa katika
Magereza na shule za sekondri badala ya kutegemea Maharagwe pekee lengo likiwa
kuongeza thamani ya zao hilo ambalo limeyumba na kukosa soko kutokana na
kutegemea masoko ya nje pekee.
Waziri wa kilimo Mhe. Charles Tizeba ametoa agizo hilo
mkoani Mtwara wakati akipokea taarifa ya mkoa ambapo amesema hilo ni fundisho
na serikali haiwezi kutegemea masoko ya nje pekee.
Amesema maeneo kama Magereza na shule za sekondari hazina
budi kutumia kitoweo hicho badala ya kutegemea maharagwe pekee lengo likiwa
kuongeza thamani ya zao hilo ambalo kwa sasa halina soko.
Hata hivyo amesema serikali kwa sasa inafanya mikakati ya
kupata masoko katika nchi zingine ikiwemo Morishas baada ya nchi ya India
ambayo ilikuwa mnunuzi mkuu wa zao hilo kuzalisha kwa wingi zao hilo katika
msimu uliyopita.
Akiwa mkoani Mtwara Mhe. Tizeba ametembelea pia kituo cha
utafiti wa kilimo Naliendele ili kujionea shughuli zinazofanywa na kituo hicho,
sambamba na kutembelea bandari ya Mtwara kujionea usafirishaji wa Korosho
kwenda nje ya nchi unavyo fanyika
Post a Comment