Treni yagonga lori na kushika moto Afrika Kusini
Treni ya kubeba abiria imeshika moto baada ya kugongana na lori nchini Afrika Kusini.
Maafis awanasema watu 12 wamefariki na wengine 268 kujeruhiwa.
Maafis awanasema watu 12 wamefariki na wengine 268 kujeruhiwa.
Mkanda wa video umeonesha behewa moja la treni hiyo likiwa linawaka moja, pembeni kukiwa na gari lililopondwa pamoja na lori lililopinduka.
Abira ambao waliokolewa kwenye treni hiyo walikuwa pembeni na mizigo yao wakiwa wamekwama.
Ajali hiyo ilitokea karibu na mji wa Kroonstad katika jimbo la Free State baada ya lori kukosa kusimama katika makutano ya barabara na reli.
Baadhi ya abiria walinusurika bila majeraha
Polisi wamenukuliwa wakisema abiria 850 wameondolewa kutoka kwenye treni hiyo wakiwa salama.
Post a Comment