Ukosefu wa damu katika hospital ya bombo wafika mwisho
![]() |
Mratibu wa huduma za maabara mkoa wa TANGA,MUSSA JUMA KAYANDA akiongea mwandishi wa MAJLIS MEDIA mapema leo |
Hospital
ya rufaa ya mkoa wa TANGA BOMBO inatarajia kuanzisha mpango kabambwe wa kuhakikisha
huduma ya upatikanaji wa damu salama katika hospital zote za serekali mkoani
hapa inaimarika kwa kiwango kikubwa zaidi.
Aidha,mpango huo ni kuvishirikisha zaidi vituo
binafsi vya afya na kwa kila kituo kitaratibu zoezi la uchangiaji wa damu kwa
kila mwezi kwa lengo la kupata Uniti 200 za damu huku mpango huo ukitarajiwa
kuanza ndani ya mwezi huu january.
Mratibu wa huduma za maabara mkoa wa TANGA,MUSSA
JUMA KAYANDA ameyasema hayo hii leo wakati alipokua akizungumza mubashara na MAJLIS
MEDIA kuhusu hali halisi ya upatikanaji wa huduma hiyo damu salama mkoani hapa.
Awali,akiielezea hali halisi ya bank ya damu katika mkoa
wa Tanga amesema mpaka sasa jumla ya unit 312 zipo katika banki hiyo na zinatarajiwa kutumika kwa kipindi cha wiki
mbili zijazo ndani ya mwezi huu ambao kwamchanganuao wilaya ya Pangani ina unit
26,Muheza unit 29,Handeni unit 57,Lushoto unit 10,Kilindi unit 31,Korogwe unit 42
na katika hospital ya bombo unit 125.
Mapema akitaja changamoto zinazoikabili sekta hiyo katika
mkoa wa Tanga MUSSA KAYANDA amesema kuwa ni ukosefu wa kituo maalumu cha uchangiaji wa damu salama katika mkoa ambapo hivi sasa wapo mbioni kujenga kituo nje
ya hospital ya bombo kitakachowezesha kutatua changamoto hiyo huku akiwashukuru
wananchi wanaoendelea kushiriki katika zoezi la uchangiaji wa damu katika hospital
hiyo na kutoa wito kwa wengine kuunga mkono zoezi la uchangiaji wa damu katika
hospital za serekali kwenye maeneo yao.
Mratibu huyo amesema kwa kawaida kwa kila siku
hospital za serekali katika mkoa wa Tanga kwa ujumla zinatumia unit 25 mpaka 30
za damu salama ambapo hospital ya bombo ikitajwa kuongoza kwa matumizi makubwa
ya damu kwa kutumia unit 10 na ikifuatiwa na wilaya ya Muheza sanjari na Lushoto.
Halikadhalika amewatoa hofu wananchi wa mkoa wa TANGA
kwa kusema kwamba hali ya upatikanaji wa damu salama katika hospital za serekali
kimkoa zipo za kutosha, na katika hatua nyengine amesema tegemezi kubwa la ukusanyaji wa damu hizo ni hospital ya rufaa
ya mkoa huu bombo.
Post a Comment