Wananchi TANGA watakiwa kujiunga na NHIF.
Wananchi mkoani TANGA wametakiwa kujiunga na mfuko wa taifa wa bima
ya afya (NHIF) ili kuondokana na changamoto ya ukosefu wa matibabu bora katika
vituo vya afya.
Pia wametakiwa kuwasajili watoto wao wenye umri kuanzia siku moja mpaka
kumi na minane katika mfuko wa bima ya afya wa toto afya kadi.
Bwana,ALY MWAKABABU ni meneja wa NHIF mkoa wa TANGA,ametoa wito huo
hii leo wakati alipokua akifanyiwa mahujiano mahsusi na mwahabari wa MAJLIS
MEDIA ofisini kwake.
Akizungumzia suala la mfuko wa toto afya kadi MWAKABABU amesema
jambo hilo ni agenda yao kubwa kwa sasa kimkoa ambapo wanaendelea na uwamasishaji
kwa wananchi ili waweze kukimbilia fursa hiyo na kuongeza kuwa lengo kubwa la serikali
kuleta mfuko huo ni kuwasaidia wazazi ama
walezi unafuu wa kumudu gharama za matibabu kwa watoto wao pindi
wanapougua maradhi mbalimbali.
Amesema kuwa mpaka sasa jumla ya idadi ya watoto waliosajiliwa
katika mfuko huo hawafiki hata mia tano kimkoa ambapo amesema ni idadi ndogo sana
ukilinganisha na wingi wa wananchi
waliopo katika mkoa mzima wa tanga.
Aidha,Mwakababu amesema kwamba ukosefu wa elimu kwa wananchi juu ya
umuhimu wa bima ya afya ni miongoni mwa changamoto iliyopelekea mkoa wa Tanga
kuwa na idadi ndogo ya watoto waliosajiliwa katika mfuko huo ambapo amesema
hivi sasa wanaendelea na ziara mbalimbali katika wilaya zote zilizopo mkoani
hapa kwa lengo la kuwaelimisha wananchi umuhimu wa suala hilo.
Halikadhalika,amewaomba wajasiliamali wadogo wadogo mkoani Tanga kujiunga
vikundi ili waweze kujisajili katika mfuko wa taifa wa bima ya afya NHIF katika
biashara zao ili waweze kuinusuru mitaji yao isiweze kufa kutokana na kutumia gharama
kubwa za matibabu pindi waendapo katika zahanati ama vituo vya afya.
Awali,meneja huyo wa bima ya afya mkoa wa Tanga ametumia fursa hii
kwa kupaza sauti yake kwa kuwaomba waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari
mkoani Tanga,kuisaidia serikali kuielimisha jamii kupitia vyombo vyao juu ya umuhimu
wa bima ya afya katika kaya zao wanazoishi.
Post a Comment