Watoto wawili wanusurika kufa baada ya kufukiwa

Picha wa kijana wa pili aliyezikwa hadi kifuani na babake Burundi
mtoto wa kwanza aliefukiwa mpaka kwenye kifua

Mwanamume mmoja ametoroka nchini Burundi baada ya kuwapa adhabu ya kikatili watoto wake wawili ambao inadaiwa aliwapata wakiiba mahindi kwenye shamba lake.
Mwanaume huyo aliwazika ardhini wanawe wawili hadi sehemu ya vifua kabla ya kuwachapa viboko,Tukio hilo la ajabu lilitokea katika kijiji cha Bubanza, mkoa wa kaskazini magharibi mwa mji mkuu Bujumbura Jumapili jioni.

Kijana aliyezikwa hadi kifuani na babaake
mtoto wa pili aliefukiwa
Taarifa zinasema watoto hao wenye umri kati ya miaka 8 na 10 walikamatwa wakiwa wanaiba katika shamba la mahindi.Walibahatika kuokolewa na mpita njia ambaye alikuwa jirani yao Mmiliki wa shamba hilo aliamua kuchimba mashimo mawili na kumzika kila mmoja wao hadi usawa wa vifua vyao na kuanza kuwatandika viboko.
Wakazi wa eneo hilo wanasema kuwa hawajui ni nini kingetokea kwa watoto hao kama jirani yao asingepita,Mwanaume huyo kisha alitoroka na watoto hao wakaokolewa.
Polisi wanasema bado wanamsaka mwanaume huyo kwa ajili ya kumfikisha mbele ya sheria,Si mara ya kwanza kwa tukio la aina hii la kikatili dhidi ya watoto kufanyika nchini Burundi.
Watoto wawili walikatwa mikono yao ya kushoto katika jimbo la kati la Gitega mwezi Novemba mwaka jana baada ya kupatikana wakiiba mahindi.

No comments