Dkt. Shein awahimiza Wazanzibar kudumisha usafi wa mazingira
Rais wa Zanzibar, Dkt Ali Mohammed Shein amewataka wakazi wa Mkoa wa Mjini Magharibi kuhakikisha wanadumisha usafi wa mazingira katika maeneo yao ili kujikinga na maradhi mbalimbali ikiwemo magonjwa ya milipuko.
Rais Shein ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa shughuli za usafi wa mazingira ikiwa ni miongoni mwa Shamrashamra za kuelekea maadhimisho ya sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Zanzibar inatarajia kuadhimisha Mapinduzi matukufu ya Mwaka 1964, huku suala la usafi wa mazingira katika maeneo ya mijini likisisitizwa ili kuuweka mji wa Zanzibar katika haiba ya kupendeza.
Aidha Dkt Shein amesema Serikali haiko tayari kuona baadhi ya watu wanayabeza Mapinduzi kwani ushahidi uko wazi kuwa Zanzibar imepiga hatua za maendeleo kutokana na Mapinduzi hayo ya mwaka 1964.
“Kila nchi inajengwa na watu wake wenyewe, na sisi tunaijenga Zanzibar wenyewe, miaka 54 tumeianza leo tangu Zanzibar tumeikomboa, hatua tuliyoifikia ni kubwa sana tangu Zanzibar tuikomboe.”
Alisema Dkt. Shein.
Utekelezwaji wa agizo la rais kuhusu usafi wa mazingira limeungwa mkono na wananchi walioshiriki shamrashara hizo za maandalizi ya maadhimisho ya sikukuu za Mapinduzi waliojitokeza katika siku hiyo ya usafi ambao baadhi wamewataka wenzao kutopuuza agizo za rais la kusimamia usafi katika miji yao huku wengine wakiiomba sereikali
kuzitolea ufafanuzi sheria ndogondogo za utunzaji mazingira.
Shughuli hiyo ya usafiri imefanyika katika eneo la nyumba za wazee Sebleni.
Post a Comment