Naibu wazir wa maliasili na utalii awaagiza wakuu wote wa wilaya kupanda miti milioni 1.5 katika kila wilaya
Naibu wazir wa maliasili na utalii ,mheshimiwa
japhet hasunga amewaagiza wakuu wote wa wilaya nchini
kuhakisha wilaya zao
zinapanda miti milioni 1.5 kwa vitendo kama sheria inavyoelekeza na si
ubabaishaji.
Mheshimiwa hasunga
ametoa kauli hiyo alipokua akizungumza kwa njia ya simu na mwanahabari wa radio
nuur fm hii leo.
Amesema sheria
inaelekeza kwa kila wilaya iweze kupatanda miti milioni 1.5 kwa kila mwaka
lakini asilimia kubwa za wilaya zimekua zikikiuka sheria kwa kufanya
ubabaishaji mkubwa ambapo wanaonyeshamiti walioipanda katika makaratasi
na si kiuhalisia wa miti yenyewe iliyopandwa.
Aidha,amesemaendapo
miti hiyo itapandwa katika kila wilaya kutapunguza wimbi kubwa linaloonekana
sasa la uharibifu wa misitu ya asili kwenye maeneo mbalimbali nchini.
Katika hatua nyengine
mheshimiwa naibu waziri huyo wa maliasili na utalii amesema kutokana na hivi
sasa asilimia kubwa ya misitu kutotoa mapato stahiki katika nchi,serikali
imejipanga kuanzisha viwanda vitakavyotegemea malighafi za misitu,kuandaa
mpango kabambe wa utoaji vibali vya kusafirisha malighafi za misitu nje ya
nchi ili sekta hiyo iwe tegemezi katika kuliingizia taifa mapato
Post a Comment