Benazir Bhutto katika eneo la kampeni ya uchaguzi muda mfupi kabla ya kuuawaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionBenazir Bhutto katika eneo la kampeni ya uchaguzi muda mfupi kabla ya kuuawa
Benazir Bhutto alikuwa mwanamke wa kwanza kuongoza taifa la Kiislamu .
Muongo mmoja baada ya mauaji yake umebaini yalioendelea Pakistan zaidi ikiwa kuusu aliyeagiza njama za mauaji yake.
Bhutto aliuawa mnamo tarehe 27 Disemba 2007 na mlipuaji wa kujitolea muhanga mwenye umri wa miaka 15 kwa jina Bilal.
Alikuwa amemaliza kampeni zake za uchaguzi katika mkutano wa kisiasa katika eneo la Rawalpindi wakati alipokaribia msafara wake akampiga risasi na kujilipua .
Bilal aliagizwa kutekeleza shambulio hilo na kundi la wapiganaji la Pakistan Taliban.
Benazir Bhutto alikuwa mwanawe wa kike Zulfikar Ali Bhutto , waziri mkuu wa kwanza Pakistan aliyechaguliwa kwa njia ya kidemokrasia .
Uongozi wake ulimalizwa baada ya kunyongwa na utawala wa kijeshi wa jenerali Zia-ulHaq. Benazir aliendelea na kuwa waziri mkuu mara mbili 1990, lakini hakuaminiwa na jeshi ambalo lilitumia madai ya ufisadi kumuondoa madarakani.
Wakati wa kifo chake, alikuwa akijiandaa kuwania muhula wa tatu kama waziri mkuu. Mauaji yake yalisababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Pakistan.
Wafuasi wa Bhutto walifanya maandamano na kufunga barabara na kuwasha moto huku wakiimba nyimbo za kupinga mauaji ya kiongozi wao.
Shambulio hilo lilitokea sekunde chache baada ya picha yake kupigwa.Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionShambulio hilo lilitokea sekunde chache baada ya picha yake kupigwa.

Jenerali na simu ya kutishia.

Muongo mmoja baadaye ,jenerali aliyekuwa akisimamia Pakistan wakati huo alikuwa amependekeza kwamba kuna watu katika utawala wake ambao walihusika na mauaji hayo.
Alipoulizwa iwapo kuna watu wabaya walioshirikiana na Taliban kuhusu mauaji hayo , Jenerali Pervez Musharraf alijibu: kuna uwezekano. Kweli. Kwa sababu jamii imegawanyika katika misingi ya kidini.
Na alisema watu hao huenda walihusika na mauaji yake. Ni taarifa ya kutatanisha kutoka kwa kiongozi wa zamani wa Pakistan .
Kawaida viongozi wa jeshi nchini Pakistan hukana madai yoyote kuhusu maoni ya ushirikiano wa serikali katika mashambulizi ya kijeshi ya jihadi.
Pervez Musharraf alikana kumtishia Bhutto katika simu
Image captionPervez Musharraf alikana kumtishia Bhutto katika simu
Alipoulizwa iwapo alikuwa na habari fulani kuhusu watu serikali anaodai huenda walihusika katika mauaji hayo, alisema: Sina ushahidi wowote.
Lakini maoni yangu ni wazi.. nadhani mwanamke anayeonekana kulemea upande wa mataifa ya magharibi huchukiwa sana na watu kama hao.
Musharraf yeye mwenyewe alishatakiwa kwa mauaji, kuhusika katika vitendo vya uhalifu kwa lengo la mauaji mbali na kusaidia kutekeleza mauaji kuhusiana na kesi ya Bhutto.
Waendesha mashtaka wanasema kuwa alimpigia simu Benazir Bhutto mjini Washinton tarehe 25 Septemba , wiki tatu kabla ya kukamilisha maficho yake ya miaka minane.
Msaidizi wa muda mrefu wa Bhutto Mark Seighal na mwandishi Ron Suskind wote wanasema waliandamana na Bhutto wakati simu hiyo ilipopigwa kulingana na Seighal muda mfupi baada ya simu hiyo.
Bhutto alisema: alinitishia. Aliniambia nisirudi, alinionya nisirudi. Musharraf alisema kuwa hatawajibika na kitakachomfanyikia Bhutto iwapo atarudi, Seighal aliambia BBC.
Na alisema kuwa usalama wake utategemea uhusiano wao. Musharraf amekana kupiga simu hiyo na kupinga wazo kwamba huenda aliagiza mauaji yake.
Kwa kweli nilicheka, aliambia BBC hivi karibuni..Kwa nini nimuue?

Njama kali

Kesi dhidi ya Musharraf imekwama kwa sababu alitorokea mafichoni mjini Dubai.
Mwana wa Benazir Bhutto ambaye amemrithi mamake kisiasa Bilawal amekana matamshi ya Musharraf.
Musharraf alitumia kila njia ili kumuua mamangu, alisema. Kwa makusudi alihujumu usalama wake ili auawe na kuondolewa katika eneo la muaji.
Bomu lililipuka karibu na gari la aliyekuwa waziri mkuu Benazir Bhutto tarehe 27 Disemba , 2007 kufuatia mkutano wa kisiasa katika eneo la Rawalpindi, Pakistan.Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAlimpiga risasi Bhutto kabla ya mlipuko kutokea.
Huku kesi ya Musharraf ikiwa imekwama , wengine wameachiliwa kwa kutenda uhalifu huo .
Katika wiki chache za mauaji hayo washukiwa watano walikiri kumsaidia kijana huyo wa miaka 15 Billal kumuua Bhutto kutokana na maagizo ya kundi la Taliban la Pakistan na lile la al-Qaeda.
Mtu wa kwanza kukamatwa , Aitzaz Shah, aliambiwa na kundi la Taliban la Pakistan kwamba ndiye atakayekuwa mlipuaji wa kujitolea aliyechaguliwa kumuua Bhutto.
Lakini baadaye akawekwa kama mlipuaji wa ziada iwapo jaribio la shambulio hilo litafeli.
Washukiwa wengine wawili Rasheed Ahmed na Sher Zaman , walikiri walikuwa wakipanga njama hiyo pamoja na binamu wao wawili katika eneo la Rawalpindi Hasnain Gul na Rafaqat Husain.
Waliambia mamlaka kwamba walitoa nyumba ya kulala ya Bilal usiku kabla ya mauaji hayo.
Benazir Bhutto akifanya kampeni za uchaguzi katika eneo la Mirpur Khas, Pakistan, tarahe 18 Disemba 2007Haki miliki ya pichaAFP
Benazir Bhutto akifanya kampeni za uchaguzi katika eneo la Mirpur Khas, Pakistan, tarahe 18 Disemba 2007Haki miliki ya pichaAFP
Hata iwapo ushahidi huo ulifutiliwa mbali , rekodi za simu zilionyesha maeneo ya washukiwa hao pamoja na mawasiliano yao saa chache kabla ya mauaji ya bi Bhutto .
Hasnain Gul aliwapeleka maafisa wa polisi na kuonyesha ushahidi katika nyumba aliokuwa akiishi.
Chembechembe za DNA kutoka mwili wa Bilal uliokusanywa baada ya shambulio hilo kabla ya kupimwa katika maabara zilithibitisha chembechembe kama hizo katika viatu vya mazoezi, kofia, na nguo ambayo Bilal alikuwa ameiwacha nyuma katika makaazi ya Husnain wakati alipovaa vesti ya kujilipua,

No comments