ASKARI WALA RUSHWA TANGA KUKIONA CHA MTAMA KUNI
TANGA.
Kamanda wa Jeshi la Polisi
mkoa wa TANGA, kamishina msaidizi mwandamizi wa Jeshi la Polisi EDUARD BUKOMBE
amewataka wananchi kuwafichua askari Polisi wanaojiusisha na vitendo vya rushwa
huku akitoa rai kwa askari wenye mchezo huo kujitathimini upya kama
wanastahili kuwa wahudumu wa jeshi hilo.
Kamanda BUKOMBE ametoa kauli
hiyo ofisini kwake wakati alipokua
akifanyiwa mahujiano mahsusi na MAJLIS MEDIA ambapo amesema kanuni na sheria za utumishi
haziruhusu mtumishi wa umma kujiusisha
na vitendo vya rushwa na kusema katika nafasi yake hatoweza kumvumilia mtumishi
wa Jeshi hilo anaejiusisha na vitendo hivyo.
Aidha amewataka wananchi
kutoa taarifa za viashiria vya uvunjifu wa amani katika maeneo yao huku akitaja
mipango mikakati ya Jeshi lake ni kuwa karibu zaidi na wananchi ili suala la
ulinzi na usalama liwe ni la kila mtanzania na si Jeshi la Polisi pekee.
Hata hivyo amesema wameanzaa
doria katika maeneo ya bahari kwa lengo la kutokomeza biashara za magendo huku
akisema matukio ya uingizwaji na ukamataji wa madawa ya kulevya yamepungua kwa
kiasi kikubwa.
Post a Comment