JESHI LA POLISI MKOANI TANGA,LIMEKUSANYA BILIONI TISA
Jeshi la polisi mkoani
TANGA,limekusanya Bilioni 9,238,6,27,000 kutokana na makosa ya usalama
barabarani kwa mwaka 2017 mkoani hapa.
majlismedia.blogespot.com
Akizungumza hii leo katika maadhimisho
ya siku ya usalama barabarani kimkoa katika viwanja vya tangamano jijini hapa,mkuu
wa kikosi cha usalalma barabarani mkoa wa TANGA,RTO SADIK RAMADHAN MSANGI
amesema fedha hizo zinatokana na ukamataji wa makosa kuanzia kipindi cha
januari mpaka November ambapo walifanikiwa kukamata makosa 39,860 na makosa 36,511
yalitozwa faini ya papo kwa papo na kupelekea ukusanyaji wa fedha hizo.
Amesema takwimu zinaonyesha kwamba
mwaka 2017 makosa yamezidi ukilinganisha
na mwaka uliopita wa 2016 ambapo kwa kipindi hicho cha January mpaka November yalikua makosa 35,444,na
makosa 32,235 yalitozwa faidi za papo
hapo na kufanikiwa kukusanya kiasi cha pesa Milioni 975,8,20,000.
Aidha,amesema kwa upande wa ajali za barabarani kwa mwaka huu 2017 zimepungua
kutoka ajali 91 mwaka jana hadi ajali 70 mwaka huu,ambapo ajali zilizosababisha
vifo kwa mwaka 2016 zilikua 67 na mwaka 2017 zilikua 53 na kusababisha vifo vya
watu 86 kwa mwaka 2016 na watu 59 mwaka 2017,na kwa upande wa majeruhi kwa
mwaka 2016 walikua 170,na 2017 walikua 112.
MSANGI ametaja mikakati
mathubuti juu ya kuzithibitia ajali hizo kuwa ni kuongeza
jitihada za kutoa elimu mashuleni na kwa madereva wa vyombo vya moto sanjari na
kuongeza jitihada katika usimamizi wa sheria za usalama barabarani katika
mkoa.
Awali mgeni rasmi wa
maadhimisho hayo ambae ni kaimu mkuu wa mkoa wa tanga,ambae ni mkuu wa wilaya
ya muheza mkoani hapa,Mhandisi.MWANAASHA RAJABU TUMBO amewapongeza askari wa
jeshi la polisi katika usimamizi wa sheria za usalama barabarani huku akiwataka
kuongeza juhudi katika kukemea vikali madereva wazembe wanaoendesha
usafiri wakiwa wamelewa.
Post a Comment