Kata ya MABOKWENI yakabiliwa na changomoto za elimu.
Shule za msingi KIRUKU,MABOKWENI na KIBAFUTA
zilizopo kata ya MABOKWENI jijini TANGA,zinakabiliwa na changamoto mbalimbali
za kitaaluma hali inayosababisha wanafunzi kushindwa kupata elimu bora katika
shule hizo.
Miongoni mwa changamoto zilizopo katika shule
hizo ni uchakavu wa miundombinu ya madarasa ambapo kuna baadhi ya madarasa
yameonyesha nyufa kubwa jambo linalohatarisha usalama wa maisha ya wanafunzi na
walimu shuleni hapo huku suala la uchache wa miundombinu ya madarasa kwa
wanafunzi wa darasa la kwanza likijitokeza hali inayowalazimu wanafunzi
kurundikana katika darasa moja na kusababisha usumbufu mkubwa kwa walimu wakati
wa ufundishaji.
Aidha,mbali na changamoto hizo pia shule hizo
zinakabiliwa na tatizo la uchache wa matundu ya vyoo,ukosefu wa milango kwa
baadhi ya madarasa,uchakavu wa nyumba za walimu wakuu sambamba na ukosefu wa
ofisi za walimu kwa baadhi ya shule hizo.
Hayo yamebainishwa hii leo na mwanahabari mwandamizi
wa MAJLIS MEDIA alipofanya ziara ya
kuzitembelea shule hizo kwa lengo la kujionea hali ya mwitikio wa wanafunzi
kipindi hiki cha mwezi January katika kata hiyo ya Mabokweni jijini Tanga.
Mwanahabari huyo mwandamizi wa MAJLIS MEDIA
amemtafuta Diwani wa kata hiyo ya MABOKWENI kupitia tiketi ya chama cha
wananchi CUF,Mheshimiwa JUMA RAMADHANI ,ambapo kwa upande wake amesema kuwa
changamoto hizo zipo kwa muda mrefu lakini hakuna hatua za awali zilizochukuliwa
kutoka kwa viongozi husika wa halmashauri ya jiji la TANGA juu ya kutafuta
utatuzi wa changamto hizo kwenye shuel hizo.
Aidha,ametumia nafasi hii kwa kumuomba
mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya jiji la Tanga,Bwana DAUDI MAYEJI kuweka
bajeti ili kuzitatua changamoto hizo.
Katika hatua nyengine MAJLIS MEDIA ilipotaka
kuzungumza na walimu wa shule hizo kwa upande wao waligoma kuzungumza chochote
hadi hapo watakapopata kibali maalumu kutoka kwa mwajiri wao ambae ni
mkurugenzi wa jiji la Tanga DAUDI MAYAJI huku MAJLIS MEDIA ikifanya jitihada za
makusudi za kumpata mkurugenzi wa jiji la Tanga ama afisa elimu wilaya ili
aweze kuzizungumzia changamoto hizo na kujua hatima ya ufumbuzi wake katika
shule hizo.
Awali MAJLISI MEDIA imejionea
hali ya uandikishwaji wa wanafunzi wa darasa la kwanza katika shule hizo ambapo
hadi sasa katika shule ya msingi MABOKWENI imekwishaandikisha wanafunzi 99 wa
darasa la kwanza ambako wanaume 52,wanawake 47 ,shule ya KIRUKU imeandikisha
wanafunzi 27 ,wanaume 21 na wanawake 6 na shule ya msingi KIBAFUTA imeandikisha
wanafunzi 50,wanaume 30 na wanwake 20.
Post a Comment