Viongozi Rukwa waanza kutatua tatizo la uhaba wa madarasa
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo, leo Jumapili ameshirikiana na wananchi wake, katika ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Sekondari ya Kirando ambayo imepangiwa kuchukua wanafunzi 422 huku uwezo wake ukiwa ni wanafunzi 200.
Mbali na mkuu huyo wa mkoa, naye Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Said Mtanda ameshiriki katika kampeni hiyo ya nguvu kazi na vifaa vya ujenzi kwa lengo la kufanikisha wanafunzi waliopata nafasi ya kuingia kidato cha kwanza kuanza masomo ili kutimiza ndoto zao.
Viongozi hao walikusanyika pamoja na wananchi wa maeneo hayo katika ujenzi huo ambao unalenga kusaidia kupunguza adha na upungufu wa uhaba wa madarasa kwa mkoa huo.

Post a Comment