Baba Ampigisha mwanae kwato hadi kufa

mtoto Benedicto Salumu (13), mkazi wa Kitongoji cha Saint Maria Kata ya Matai  wilayani Kalambo mkoani Rukwa, inadaiwa amepigwa na baba yake hadi kufa baada ya ugomvi kuzuka kati ya mama na baba wa mtoto huyo.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kitongoji hicho, Rafael Sinyangwe, amesema tukio hilo lilitokea Januari 1 saa 4 usiku,kwani kwa muda mrefu kumekuwapo ugomvi baina ya baba wa mtoto, Pius Salum (46) na mkewe, Hilda Mpangamila (37), akimtuhumu mkewe kuwa mtoto huyo si wa kwake.

Mwenyekiti huyo amesema Salum mara kadhaa amekuwa akiwalalamikia ndugu zake kuwa mkewe alibeba ujauzito wa mtoto huyo wakati akiwa amekwenda kutafuta maisha na aliporudi alihisi mkewe ni mjamzito.

Mwenyekiti Sinyangwe alidai siku ya tukio hilo mtuhumiwa akiwa ametoka kusherehekea Mwaka Mpya, aliingia chumbani na kukuta mtoto huyo akiwa amelala kisha kuanza kumpiga  ngumi na mateke sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwamo tumboni hadi kusababisha kifo chake.

Aliendelea kudai kuwa baada ya kumua, alimpiga pia mke wake akidai amemsababishia kulea mtoto asiyekuwa wake kwa muda mrefu, hali mbayo ilikuwa ikimuudhi na kumkosesha amani.

Kamanda wa Polisi mkoani Rukwa, George Kyando, amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo na Kuongeza kuwa mtuhumiwa anashikiliwa na jeshi la polisi na atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazo mkabili.

No comments