Serikali mkoani TANGA yatumia zaidi ya Bilioni 30.


Serikali mkoani TANGA,imetumia Bilioni 30,416,058,340.92 katika utekelezaji wa mpango wa kunusuru kaya masikini nchini TASAF III kwa walengwa 55,703 wa mpango huo mkoani hapa.

Katibu tawala mkoa wa TANGA,Mhandisi.ZENA SAID ameyasema hayo alipokua akizungumza na MAJLIS MEDIA ofisini kwake.

Awali Mhandisi.ZENA amesema kwamba katika mkoa wa Tanga,utekelezaji wa mpango huo uliziduliwa rasmi mkoani hapa toka mwezi November mwaka 2014 na kutekelezwa katika vijiji na mitaa 681 yenye kaya 61,437,na kusema kutokana na vifo,kuhama kwa walengwa na uwepo wa kaya zisizokidhi vigezo vya kuwa walengwa ndani ya mpango,baadhi ya kaya ziliondolewa kwenye orodha ya walengwa wa mpango,hivyo hadi kufikia mwezi Noveber,2017 mpango ulikua na jumla ya walengwa 55,703 katika mkoa wa Tanga.

Aidha,katibu tawala huyo mkoa wa Tanga,amesema miongoni mwa halmashauri zilizojumulishwa na kupata mgao huo ni Tanga jiji yenye vijiji/mitaa 88,kaya 5321 ambako ilipatiwa kiasi cha fedha za mpango huo 2,870,712,500,Muheza yenye vijij/mitaa 90,kaya 7592 na kupatiwa fedha 3,552,132,954.55,Mkinga yenye vijiji/mitaa 57,kaya 4580 na kupatwa fedha za mgao 2,340,205,318.18,Pangani yenye vijiji/mtaa 35,kaya 3951 na kupatiwa 2,025,450,090.91,Korogwe yenye vijiji/mitaa 80,kaya 7724 na kupatiwa 3888075272.73,Korogwe mji yenye vijiji/mitaa 24,kaya 2894 na kupatiwa mgao wa fedha  1,538,769,431.82,Handeni yenye vijiji/mitaa 54,kaya7264 na kupewa mgao wa fedha 3,860,314,000,Handeni mij yenye vijiji/mitaa 40,kaya 2982 na kupatiwa mgao wa fedha 1,555,627,204.55.

Lushoto na bumbuli vijiji/mtaa146,kaya 6784 na kupatiwa fedha za mgao 5,072,554,886.36 pamoja na Kilindi yenye vijiji/mitaa 67,kaya 6611 na kupatiwa fedha za mgao 3,713,216,681.82 ambapo kwa mgawanyo huo ndio umefainiksha kupatikana jumla ya vijij/mitaa 681,kaya 55,703 sambamba na fedha Bilioni 30,416,058,340.92 za utekelezaji wa mpango wa TASAF III katika mkoa mzima wa Tanga.

Awali,ametaja mafanikio yaliopatikana kutokana na mpango huo kuwa ni vikundi vya kuweka Akiba na kuwekeza vimenufaika kutokana na elimu ya kuwek akiba na kuwekeza inayoendelea kutolewa na timu ya uwezeshaji ya sekretari ya mkoa kwa kushirikiana na wasimamizi wa mpango katika maeneo yautekelezaji wa kuanzia ngazi ya halmashauri.Kuanzishwa kwa vikundi vya kuweka na kukopa kutokana na kuanzishwa kashughuli za kiuchumi za ufugaji,mama lishe,kilimo chambogamboga ambazo zimewezesha kuundwa kwa vikundo vya kuweka na kukopa na kuwaongeezea kipato na kuboresha maisha ya walengwa na kuweza kujiwekea akiba.

Pia amessema kaya masikini zimeanza kuwa na uhakika wa kujikimu katika maisha yao ya kila siku na kunza kujiwekea akiba kupitia mpngo wa miradi ya kutoa Ajira ya muda wa TASAF III,Kutokana na kutolewa ruzuku ya masharti ya elimu, watoto kutoka kaya masikini wameweza kuhudhuria shule vizuri na kuongeza ufaulu katika masomo hivyo kuinua taaluma,Kupunguza idadi ya watoto wasiojua kusoma na kuandika ambao wengi wao hutoka katika kaya masikini,Kupungua kwa vifo kwa kina mama wajawazito,watoto chini ya miaka mitano na wazee kutokana na makundi hayo kupata huduma muhimu za afya kwa wakati kupitia matumizi ya bima ya afya (CHF) sanjari na kujenga uwezo wa wananchi kutoka kaya masikini kushiriki vikao mbalimbali vya matumizi katika ngazi za msingi.

Halikadhalika ameelezea changamoto zinazoukabili mpango huo ambapo ni Uwepo wa kaya nyingi masikini ambazo hazijafikiwa na mpango huo kutokana na upungufu wa wa rasilimali fedha,Baadhi ya walengwa wa mpango kufutwa kimakosa kwenye orodha ya malipo bila ya maelezo hivyo kukosa haki ya kupata fedha za kujikimu pamoja na walengwa wengi wa mpango huo hasa katika maeneo ya vijijini wazee wasio na uwezo wa kutumika (nguvu kazi) katika uzalishaji ,hivyo ruzuku wanazopatiwa ni kwa ajili ya chakula na sio kujiongezea kipato kwa njia ya kuwekeza katika miradi ya kiuchumi.

Mhandisi ZENA SAIDI amesema kuwa serikali ya mkoa wa Tanga itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ndani ama nje ya mkoa ili kuhakikisha kwamba malengo ya TSAF III kuzinusuru kaya masikini yanafikiwa.


No comments