Huduma ya maji safi jiji TANGA pasua kichwa
Hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika halmashauri
ya jiji la TANGA,imeanza kuadimika hali inayosababisha adha kubwa kwa wananchi
kutokana na ukosefu wa huduma hiyo.
MAJLIS MEDIA imebainisha hayo hii leo wakati ilipofanya ziara kwa
nyakati tofauti katika kata za MSAMBWENI,MABAWA,DUGA,MAGAONI,TANGASISI,
MNYANJANI sambamba na MASIWANI zilizopo jijini
Tanga na kujionea hali halisi ya huduma hiyo ikisuasua kutoka kwenye vizimba vya
maji.
Mapema wakizungumza na MAJLIS MEDIA baadhi ya wananchi wa kata hizo wamesema kwamba toka mwezi January ulipoanza mwaka
huu suala la huduma ya maji kwenye maeneo yao imekua ni chamgamoto kubwa
kuipata huduma hiyo.
Wamesema ukosefu wa maji umesababisha adha kubwa kwao ambapo baadhi yao hutumia
gharama kubwa kununua maji ya dukani kwa mahitaji ya nyumbani na huku wegine
wakisema kwamba hutumia muda mwingi kwenda visimani kufuata huduma hiyo hali
inayo sababisha kutofanya shughuli za kimaendeleo katika nyumba zao.
Aidha,wananchi hao wameitupia lawama mamlaka ya maji safi na usafi wa
mazingira jijini Tanga,(TANGA UWASA) kwa kushindwa kutoa taarifa mapema juu ya
changamoto hiyo.
MAJLIS MEDIA imefika katika ofisi za mamlaka hiyo ambapo kwa upande wake
mkurugnzi wa mamlaka hiyo Mhandisi.FARLES ARAM amesema kuwa tatizo liliosababisha
kutokea kwa hali hiyo ni kukatika katika kwa umeme ambapo imesababisha kutokea
tatizo la ghafla kwenye njia kuu ya kupeleka umeme eneo la mtambo wa kutibu
maji uliopo MOWE na kusababisha mtambo wa kutibu na kusukuma maji umesimamisha
uzalishaji wa majisafi kutokana na tatizo hilo.
Post a Comment