Madereva wakatao ruti jijin Dar esa laam kukiona cha moto

Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi kavu na majini SUMATRA imefanya mabadiliko ya mzunguko wa mabasi ya daladala jijini Dar es Salaam katika kituo cha mabasi cha Mbezi mwisho lengo likiwa ni kudhibiti madereva wa daladala kukatisha safari na kusababisha adha kubwa kwa abiria.
Akizungumza wakati akitoa taarifa hiyo kwa madereva pamoja na wamilikiwa daladala kaimu Mkurugenzi Mkuu Sumatra Johansen Kahatano amesema mabadiliko hayo yatasaidia kuboresha huduma za usafirishaji wa abiria kwa kuongeza upatikanaji wa huduma pamoja na kuondoa kero za ukatishwaji wa njia ,utozaji wa nauli zisizoridhiwa na mamlaka pamoja na msongamano kwenye vituo vya daladala.
Bwana Kahatano amesema utekelezaji wa njia hizo utafanyika kwa awamu tofauti ambapo njia namba moja itahusisha magari yatakayotoka mbezi luis au kibamba shule kwenda makumbusho au Kawe kupitia barabara ya Morogoro na wakati wa kurudi mbezi luis au kibamba shule kupitia Goba ambapo njia namba mbili itahusisha magari yatakayoanzia mbezi luis kwenda makumbusho au kawe kupitia goba na wakati wa kurudi mbezi luis kibamba shule ,kupitia barabara sam nujoma na morogoro.
Kwa upande wao wamiliki pamoja na madereva wa daladala wamesema wamepokea mabadiliko hayo na kuhaidi kutekeleza ikiwemo kufuata sheria zilizopo.

No comments