Mbowe akerwa na lowasa,atema cheche
Muda mfupi
baada ya Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Edward Lowassa kukutana na kufanya
mazungumzi na Rais Dkt John Pombe Magufuli na kusifu utawala wake, Mwenyekiti
wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe amezungumza na kusema kuwa, kauli iliyotolewa
na Lowassa wakati wa ziara yake ya Ikulu leo, sio msimamo cha chama hicho.
Lowassa
ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, amekutana na Rais Dkt Magufuli Ikulu
na kumsifu kwa namna anavyoiongoza nchi pamoja na kutekeleza miradi mikubwa
ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), mradi mkubwa wa kufua umeme wa
Strigler’s Gorge ambayo kwa pamoja itaongeza ajira kwa wananchi.
Mbowe
akizungumza na Radio Deutsche Welle (DW amesema kuwa huo sio msimamo wa chama
chao, kwa sababu wao hunafanya maamuzi kupitia vikao, na hutoa maazimio ya
pamoja baada ya kutafakari na kujadiliana kwa upana wake kila hoja.
Aidha, Mbowe
ametaja matukio mbalimbali yanayopelekea kukandamiza demokrasia nchini, watu
kupotea na wengi kuokotwa wakiwa wamekufa, huku uchumi pia ukikidima na kuhoji
mtu anatoa wapi ujasiri wa kupongeza serikali ya awamu ya tano, chini ya Rais
Dkt John Pombe Magufuli.
Post a Comment