Wanafunzi zaidi ya 500 wakosa pakusomea mkoan mbeya
Wanafunzi zaidi ya 500 wanaosoma katika shule ya msingi Chunya Mjini Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya, hawana mahala pa kijifunzia baada ya paa la vyumba vitano vya madarasa na kimoja cha walimu kuezeliwa na upepo ulioambatana na mvua .
Chanzo za khabari kimefika katika shule ya msingi Chunya Mjini na kujionea halio ilivyo, na kuzungumza na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Agnetha Pius Nchimbi ambapo amesema , kuezuliwa kwa shule hii hakukuleta madhara yeyote kwa wanafunzi kwa kuwa ulikuwa ni muda ambao wanafunzi wote walikuwa majumbani, na alibaki peke yake ofisini akiendelea na majukumu ya kazi, na kwamba ilianza kunyesha mvua ikiambatana na upepo, na hivyo kuezua vyumba vitano vya madarasa na chumba kimoja kinachotumia na walimu.
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Rehema Madusa anasema kuezuliwa kwa shule hiyo, kumesababishwa na kujengwa chini ya kiwango na hivyo kukosa ubora, na kwamba kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, baada ya kubaini hilo imeaamua kuiboresha ili kuepuka madhara kama hayo hapo baadae.
Kutokana na Tukio hili Mfuko wa Tulia Trust Fondation unaomilikiwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Tulia Akson Mwansasu, umekabidhi msaada wa bati 100, wakati huo pia Mbunge wa jimbo hilo nae akitoa bati 100.
Post a Comment