Serikali yaombwa kuruhus uchimbaji madini
Wachimbaji wadogo wadogo wa madini mkoani Tanga,
wameiomba serikali kuruhusu maeneo yenye madini kuchimbwa ili wananchi waweze
kujipatia kipato na kuendelea kiuchumi.
Wakizungumza na MAJLIS MEDIA, mapema leo hii,
wachimbaji hao wadogo wamesema tanga ni miongoni mwa mikoa yenye ardhi iliyo na
madini lakini bado yamezuiwa kutochimbwa tangu kugundulika na kusababisha hali
ya uchumi kwa wananchi kupungua kwa kiasi kikubwa.
Wakizungumza kwa hisia kali wachimbaji hao wamemwomba
waziri mwenye dhamana wa wizara ya madini kufuatilia maeneo yote katika wilaya
tofauti mkoani hapa ili kuruhusu wachimbaji kuchimba madini hayo kwa kufuata
utaratibu wa kisheria.
Aidha wamesema kuna maeneo ambayo hayawezi kuleta
athari yeyote kimazingira lakini wanashangaa kuona wamezuiliwa kuchimba jambo
ambalo linawakatisha tamaa katika kupiga hatua za kimaendeleo.
Wameongeza kuwa mikoa mingi ya bara inagundulika
migodi kila wakati lakini viongozi husimamia na kuruhusu wachimbaji wadogo
kuendelea na shughuli za uchimbaji tofauti na mkoa wa Tanga ambapo maeneo mengi
yaliyojitokeza madini yamezuiliwa mpaka muda huu ukiachilia mbali yale yaliyopo
katika vyanzo vya maji na misitu ya hifadhi.
Post a Comment