Wajawazito na wazaz Bombo walia na wahudumu
Baadhi ya wahudumu wa afya katika hospital ya rufaa ya mkoa wa
TANGA BOMBO,bado wanaendelea kulalamikiwa na wananchi kutokana na tabia yao ya utoaji
lugha zisizokua na staha kwa wagonjwa hospitalini hapo.
Wakizungumza na MAJLIS MEDIA hii leo baadhi ya wagonjwa na wananchi
hospitalini hapo wamesema kwamba licha ya rais wa jamuhuri wa muungano wa
Tanzania Dkt JOHN POMBE MAGUFUL kujitahidi kuleta nidhamu kwa watumishi wa umma
kwa kukemea vikali wafanyakazi wazembe na wanaokiuka sheria na kanuni za
utumishi bora wa kazi za umma kwa kuwanyanyasa wananchi bado tatizo hilo
linaendelea kwa baadhi ya wafanyakazi wa afya katika hospita hiyo.
Aidha,wamesema kwamba miongoni mwa hodi iliyotawaliwa na vitendo
hivyo kwa baadhi ya wahudumu wa afya hospitalini hapo ni hodi ya wajawazito na
uzazi.
Awali mwanahabari mwandamizi wa MAJLIS MEDIA amefanya ziara hospitalini
hapo na kushuhudia baadhi ya wagonjwa wakinung’unika kwa ishara ya
kutoridhishwa na huduma za hospital hiyo ambapo kwa sauti ya juu mgonjwa mmoja
alisikika akisema kwamba ‘‘ni mara mia moja ukatibiwa hospitali binafsi kwenye
gharama kubwa kuliko kung’ang’ania hospitali hiyo ya serikali’’ ambapo alikua akimaanisha kuwa huduma
inayotolewa hospitalini hapo sio bora ukilinganbisha na hospitali binafsi.
Katika hatua nyengine wananchi na wagonjwa waliofika hospitalini
hapo wamelalamikia suala la gharama za matibabu kuwa juu katika hospitali hiyo kuliko
ubora wa matibabu yenyewe ambapo wamedai kuwa asilimia kubwa za dawa muhimu za
mgonjwa wanazoandikiwa na madaktari wanaambiwa wakanunue kwenye maduka ya dawa
binafsi.
Ikumbukwe kuwa mwishoni mwa mwaka jana mganga mkuu wa mkoa wa TANGA,Dkt
ASHA MAHITA alizungumza na MAJLIS MEDIA kwa kusema kuwa anaendelea kupokea kero
mbalimbali za wananchi juu ya namna ya kuboresha huduma za afya katika hospital
ya rufaa ya mkoa wa Tanga Bombo kupitia sanduku la maoni hospitalini hapo ama wananchi kufika ofisini kwake katika
jengo la mkuu wa mkoa wa Tanga ili wananchi waweze kupatiwa huduma stahiki ya
afya katika hospita hiyo.
Post a Comment