Mhe. Edward Ngoyai Lowassa akutana na Rais Maguful
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John
Pombe Magufuli leo tarehe 09 Januari, 2018 amekutana na kufanya mazungumzo na
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Ngoyai Lowassa, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Edward Ngoyai Lowassa amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa
kazi nzuri anayoifanya na ametaja baadhi ya maeneo ambayo kazi kubwa imefanyika
kuwa ni kutoa elimu bila malipo, ujenzi wa mradi wa uzalishaji wa umeme katika
maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler’s Gorge), ujenzi wa viwanda na ujenzi wa
reli kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge) ambavyo vinazalisha ajira nyingi
kwa Watanzania.
“Nimepata faraja sana kuja hapa Ikulu kuonana na Mhe.
Rais, tumezungumza nae na nimempongeza kwa kazi nzuri anayoifanya, lazima
tukiri anafanya kazi nzuri na anahitaji kutiwa moyo.
“Moja kubwa ambalo ni la msingi sana ni la kujenga ajira,
katika kuanza ujenzi wa reli ya kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro hapo
anajenga ajira, na kwenye nchi yoyote inayoendelea suala muhimu ni kujenga
ajira, Stiegler;s Gorge ni kujenga ajira na mingine ya aina hiyo, lazima kuwepo
na kipaumbele cha kusema kwamba tunajenga ajira, jingine ni la elimu, ni muhimu
sana, hauwezi kuacha elimu katika mambo yako unayofanya, hili nalo lazima
lisemwe vya kutosha, kwa kweli nakushukuru Mhe. Rais, you made my day” amesema
Mhe. Lowassa.
Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuli amempongeza Mhe.
Edward Ngoyai Lowassa kwa kutambua kazi kubwa inayofanywa na Serikali na
amesema Mhe. Lowassa ni mmoja wa viongozi ambaye kwa wakati wake ametoa mchango
wake katika nchi.
Mhe. Rais Magufuli ameongeza kuwa Mhe. Lowassa ni
mwanasiasa mzuri kwani hata wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita ambao
naye aligombea kiti cha Urais, hakuwahi kumtukana. “Mhe. Lowassa ameniomba mara
nyingi nikutane nae, na leo nimekutana nae, tumezungumza mambo mengi,
ameniambia ya kwake na mimi nimemwambia ya kwangu, kwa ujumla Mhe.
Lowassa ni mwanasiasa mzuri na tuendelee kuwaenzi wazee
hawa ambao kwa nyakati fulani walifanya mambo mazuri,na mimi napenda kumpongeza
Mhe. Lowassa ambaye kama alivyosema hapa kuwa tumefanya mambo mazuri mengi.
Post a Comment