Wapitishaj unga jijin tanga kukiona cha moto.
TANGA.
Kamanda
wa jeshi la polis mkoa wa TANGA, kamishina
msaidizi mwandamizi wa jeshi,SACP EDUARD BUKOMBE,ameahidi kulidhiibiti wimbi la
biashara ya madawa ya kulevya maeneo mbalimbali mkoani hapa.
Kamanda
BUKOMBE amesema dhamira hiyo imejiri kutokana na maeneo mengi mkoani hapa
kubainika uwepo wa kero nyingi za matumizi ya madawa ya kulevya ikiwemo
mirungi,bangi sanjari na madawa ya kulevya ya viwandani ambako amesema Jambo
hilo hatolifumbia macho kamwe katika nafasi yake.
Aidha,amesema
kuwa suala hilo tayali wamekwishalianza huku akiwaomba wananchi kutoa taarifa
ofisini kwake pindi wanapobaini uwepo wa watu wachache wanaojihusisha na suala
hilo ili jopo la askari wake waweze kuchukua hatua stahiki.
Awali
amesema kwamba changamoto iliopo katika suala hilo ni uwepo wa njia nyingi
za panya za usafirishaji wa madawa hayo katika mkoa ambapo amesema hivi saa
wamejipanga kikamilifu kudhibiiti njia zote hizo ikiwa kwa upande wa baharini.
RPC.BUKOMBE
amesema zoezi hilo linakwenda sambamba na suala la kuwahimiza madereva kufuata
sheria za usalama barabarani kwa kuwa kuna baadhi yao wanakiuka sheria hizo
kwa makusudi.
Hayo
ameyasema hii leo ofisini kwake wakati alipokua akifanyiwa mahujiano mahsusi na
mwanahabari wa MAJLIS MEDIA kuhusu hali ya ulinzi na usalama kimkoa.
Amesema kuhusu hali ya ulinzi na usalama katika mkoa amesema ipo shwari licha ya uwepo
wa wachache wanaoleta usumbufu lakini suala la kutii sheria bila shuruti na
kuongeza kwamba tayari amekwishaagiza vijana wake kuendelea na doria mbalimbali
kuwabaini watu hao ili wachukuliwe hatua kali za kisheria ikiwa ni kufikishwa
mahakamani.
Post a Comment