Waziri mkuu awataka wananchi walime kahawa wapate fedha
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wananchi wa wilaya ya Songea mkoani Ruvuma wajikite kwenye zao la kahawa ili wawe na zao mbadala la biashara.
Ametoa wito huo leo hii, Januari 5, 2018 wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Lipokela na vijiji jirani, wilayani Songea mara baada ya kukagua shamba la kahawa la Aviv Tanzania lenye ukubwa wa hekta 1,990.
Amesema waziri kuu Limeni kahawa ili mpate fedha sababu zao hili ni la biashara. Kahawa ni miongoni mwa mazao matano ya biashara ambayo Serikali ya awamu ya tano imeamua kuyawekea mkazo ili yaweze kuongeza tija kwa wakulima na kuinua uchumi wa Taifa.
Aidha amesema kuwa serikali imefanya tathmini na kugundua udhaifu mkubwa katika usimamizi wa mazao hayo kuanzia ngazi ya Halmashauri.
Waziri Mkuu ameendelea kusema ni lazima wananchi walime zao hilo na viongozi wahakikishe wananchi wananufaika na hata hivyo, ameonyeshwa kutoridhishwa na utendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea baada ya kuelezwa kuwa kampuni ya Aviv Tanzania imezalisha miche milioni moja lakini iliyochukuliwa na kusambazwa kwa wananchi ni miche isiyozidi 200,000.
Awali amewataka wakulima hao watenge ekari moja hadi tatu kwa kila kaya ili waweze kulima zao hilo.
Amesema itabidi zao la kahawa liundiwe mfumo maalum wa ununuzi ambao ni wa ushirika kwa kuzingatia vyama vya msingi (AMCOS) vilivyokuwepo.
Mapema, akitoa taarifa juu ya shamba hilo, Meneja wa Aviv Tanzania, Bw. Medu Medappa amesema lengo la kuanzisha mradi huo lilikuwa ni kuhakikisha wanapata shamba kubwa la kahawa aina ya Arabica nchini Tanzania lenye viwango vya kimataifa.na kuongeza kusema kuwa wamekwishatoa ajira kwa Watanzania wapatao 3,000 zikiwemo za moja kwa moja na za msimu.
Amesema kampuni hiyo imeweza kuchangia miradi ya maendeleo kwenye vijiji vinne jirani vya Lipokela, Lusonga, Liganga na Selekano. na hadi mwaka 2017 waliweza kukamilisha ujenzi wa zahanati katika kijiji cha Lipokela, nyumba za walimu katika vijiji vya Liganga na Lusonga, uchangiaji wa madawati kwenye vijiji vya Lipokela na Lusonga.
Amesema wameweza kuanzisha scheme ya wakulima wadogo wa nje (outgrowers scheme) kwa wakulima 2,000 ambao wamegawanyika kwenye vikundi 36 katika vijiji 31 ndani ya mkoa wa Ruvuma.
Waziri Mkuu anaendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Ruvuma kwa kutembelea wilaya ya Mbinga ambako atakagua miche kwenye taasisi ya TACRI, atatembelea kiwamda cha kukoboa kahawa cha Mbinga (MCCCO), kuzungumza na watumishi na madiwani na pia kuhutubia mkutano wa hadhara.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, JANUARI 5, 2018.
Post a Comment