WATU 40 WAUAWA NA WENGINE KUJERUHIWA KAABUL
Kiasi cha watu 40 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika msururu wa milipuko ya mabomu iliyotokea kwenye kituo kimojawapo cha Utamaduni wa Washia mjini Kabul.
Hilo ndilo shambulizi baya zaidi la karibuni kuukumba mji huo mkuu wa Afghanistan.
ingawaje mpaka sasa hakujatolewa taarifa yoyote kuhusu aliyehusika lakini kundi la Taliban limekanusha haraka kuhusika na shambulizi hilo lililotokea karibu na Shirika la Habari la Afghanistan, ambalo ripoti za awali zilidokeza kuwa huenda ndilo lililengwa.
Nasrat Rahimi ambae ni msemaji wa Wizara ya Mambo ya ndani ameliambia shirika la habari la AFP kuwa milipuko hiyo ililenga kituo cha Utamaduni wa Kishia cha Tabayan.
Bwana Rahimi amesema mlipuko wa kwanza ulifuatwa na milipuko mingine miwili midogo ambayo haikusababisha madhara. Kundi la Taiban limeimarisha mashambulizi yake wakati kundi linalojiita Dola la Kiislamu - IS likipambana kuutanua uwepo wake nchini humo.
Post a Comment