IFIKAPO 2025 SEKTA YA UTALII KUWA TEGEMEZI
kuwa hadi ifakapo mwaka 2025 sekta ya utalii nchini itakuwa miongoni mwa sekta tegemezi katika kuliingizia taifa mapato.
Aidha amesema miongoni mwa mikakati hiyo nikuwa na ubunifu na uboreshaji wa vivutio vya taifa,pia kujikita zidi katika utalii wa utamaduni na kuunda mamlaka itakayosimamia utalii wa fukwe za bahari,kufanya maadhimisho ya mwezi wa urithi katika vivutio vya asili pamoja na kuwa na mikutano ya mara kwa mara itakayowashirikisha wadau wa masuala mbalimbali ya utalii nchini sambasamba na kuanzisha utalii wa matibabu kwenye hospital zote kubwa ikiwemo Muhimbili.
Muheshimiwa HASUNGA ameyasema hayo leo hii wakat wa ziara yake ya kikazi ya kuvitembelea vivutio mbalimbali vya utalii na maliasili vilivyopo jijini Tanga ambapo amesema hatua hiyo imejiri kutokana na hivi sasa sekta hiyo imekua ikiingiza pato dogo sana la taifa kwa mwaka ambapo huingiza milioni 17 jambo ambalo amesema linakwenda kunyume na uhalisia wa rasilimali pekee zilizopo nchini.
Awali akitoa taarifa ya sekta ya utalii kimkoa,katibu tawala mkoa wa TANGA Mhandisi ZENA SAID amesema changamoto iliyopo mkoani hapa ni wananchi kutovitumia vizuri vivutio hali inayosababisha Serikali kutoingiza pato la kutosha kupitia vivutio hivyo.
Post a Comment