Rais Magufuli awalilia wakenya walipoteza maisha kwenye ajali


Rais John Magufuli, amemtumia salamu za rambirambi rais mwenza wa Kenya, Uhuru Kenyatta kufuatia vifo vya watu 36 waliopoteza miasha baada ya basi la abiria waliokuwa wakisafiria kugongana na lori katika barabara ya Nkuru – Eldoret nchini humo. 

Katika salamu zake hizo, rais Magufuli amesema, amepokea taarifa hizo kwa mshtuko mkubwa kufuatia ajali hiyo iliyotokea mwishoni mwa mwaka 2017 na kuwapa pole familia za watu waliopoteza maisha pamoja na kuwaombea wote waliojeruhiwa kupona haraka. 

"Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko mkubwa taarifa za kutokea kwa ajali iliyosababisha ndugu zetu takribani 36 kupoteza maisha baada ya basi la abiria kugongana na lori nchini Kenya. “Msiba huu umesababisha majonzi makubwa sio tu kwa ndugu zetu wa Kenya bali pia kwetu sote wana Jumuiya ya Afrika Mashariki, tumepoteza wapendwa wetu na nguvu kazi yetu.

“Kwa niaba ya Watanzania wote nakupa pole sana ndugu yangu Mhe. Uhuru Kenyatta, Rais wa Jamhuri ya Kenya kwa msiba huu mkubwa ulioupata, nawapa pole wana familia wote waliowapoteza jamaa zao na pia nawapa pole wananchi wote wa Kenya.

No comments